|
|
| Home |
Historia ya harakati za ukombozi wa KashmirMANDHARI ya safu za milima yanayojulikana kama Jammu na Kashmir zimejilaza mipakani mwa China, India na Jamhuri ya Asia ya Kati. Safu mbili ndefu duniani za milima ya Himalayas na Karakoram ipo katika eneo hili.Mnamo mwaka 1947, wakati wakoloni wa Kiingereza wanaondoka bara dogo la India, mataifa huru ya Pakistan na India yakapatikana kwa umwagaji mkubwa wa damu kati yao. Katika kipindi hicho, asilimia 75 ya wakazi wapatao milioni nne wa Kashmir walikuwa Waislamu. Hari Singh, mtawala wa Kihindu aliyewekwa na Waingereza aliirithisha Kashmir kwa India iliyokuwa na Wahindu wengi mwaka 1947. Hata hivyo, Waingereza walikubali kwa masharti kwamba kura ipigwe kuamua matakwa ya Wakashamir. Serikali ya India ilikubali sharti, wakati huo huo yakaibuka machafuko makubwa Kashmir, vita holela kati ya India na Pakistan vikapiganwa kwa India kumwaga vikundi vya wanajeshi na Pakitan ikapeleka wapiganaji wa Kiislamu kwa upande wa Kaskazini. Matokeo ya vita hivi vya mwaka 1947 yaliifanikisha Pakistan kuteka theluthi moja ya Kashmir inayofahamika kama `Azad Kashmir' leo, wakati India inashikilia sehemu iliyobaki ikiwemo mji wa kihistoria wa Srinagar. Vilikoma vita, ikawa ndio mipaka leo hii kati ya nchi hizi, na India ikawa imeweka nguvu nyingi za kijeshi Kashmir ambapo inakaliwa na Waislamu wengi. Serikali ya India imeamua kwa makusudi kukataa maamuzi ya wananchi hao japokuwa ilikubali masharti haya mwaka 1947. Imekataa upatanisho wa baraza la usalama la umoja wa Mataifa mwaka 1948 - 1949 ambalo lilipendekeza uamuzi wa pamoja wa Wakashmir kuhusu masuala yao. Hili lilikuwa tatizo la Umoja wa Mataifa mwaka 1948, hata hivyo limebaki bila ya kupatiwa ufumbuzi hadi leo, hii inaonyesha udhaifu wa Umoja wa Mataifa. Kama hali ilivyo Pakistan, Kashmir inakaliwa na kushikiliwa na wanajeshi wasio Waislamu, wenye uadui mkubwa na Waislamu kulinda udhalimu wa serikali. Hali ilivyo Miaka ya 50 baadaye serikali ya India inayoongozwa na viongozi wenye imani ya Kihindu inaendelea kuikalia Kashmir kimabavu huku ikiendelea na vitendo vya utesaji, ubakaji na kuteketeza makazi kwa moto pamoja na kufanya mauaji ya watu wengi kwa pamoja ya Waislamu wa Kashmir. Habari ilichapishwa kwenye ukurasa wa mbele wa jarida linalotolewa na kituo cha Kiislamu ikasomeka kwa kichwa cha habari `Je tumeisahau Kashmir?' (Have we forgotten Kashmir?), dhahiri jarida hilo linatoa jibu la swali hilo kwa kuwa hawakutoa habari yoyote ndani ya jarida hilo. Kwa hakika inawezekana umma wa Kiislamu hawajui ukatili uliokuwepo kwa Wakashmir kuanzia mwaka 1947 wakati India ilipoziba masikio yake kuhusiana na matakwa ya Kashmir na Umoja wa Mataifa. Serikali ya India inajaribu kuficha ukweli na kupotosha ukweli kuhusu hali halisi, vimedhihirishwa na kuzuia vikundi vya kutetea haki za binadamu mara kwa mara. Hata hivyo juhudi za kutangaza ubaya dhidi ya wapigania uhuru wa Kashmir hazikufaa kitu kama ambavyo suala zima lilivyopewa nafasi na vyombo vya habari kwa ujumla. Miaka ya karibuni, wapanda milima raia wa Marekani na Ulaya walitekwa na kuuawa na kilichosadikika kuwa kikundi cha wapigania uhuru, ukweli ulidhihiri baada ya wanajeshi wa serikali kutajwa kuhusika na mauaji hayo. Wanajeshi hao waliendeleza vitendo vyao vya kikatili kwa watalii ikiwa ni pamoja na kumbaka mama mmoja raia wa Canada miaka michache iliyopita. Wanademokrasia wakubwa ulimwenguni wanautaka ulimwengu ugeuze macho yake kwenye mauaji hayo ambao unahusika nayo moja kwa moja. Hata hivyo Qur'an tukufu inatukumbusha:- "Hakika ukweli husimama kuliko uongo" (2:256). Takwimu zilizokusanywa na mashirika yanayojitegemea, likiwemo shirika la kutetea haki za binadamu (AI) na shirika la habari la Uingereza (Reuters) ambayo yanafuatilia ukatili na ukandamizaji Kashmir zinaonyesha kuwa, kati ya mwaka 1990- 93, takriaban Wakashmir 31,000 walipigwa risasi, vijana 30,000 waliteswa na watu wengine wapatao 300 walifungwa kamba na kutoswa katika mto Lhelum. Karibia watu 2,000 walipata ulemavu wa kudumu na 4,258 ziliathirika vibaya sehemu zao za siri kwa mateso (sexually incapacitated). Kundi la kutetea haki za binadamu la mjini Paris, Ufaransa (FIDH), liliyaelezea mateso hayo kama ni ya kikatili, kinyama na kiovu kupita kiasi. Mateso ya kifikra (mental torture) mara nyingi yakilenga kashfa (abuse), matusi ya kufedhehesha na utoaji wa hoja zinazopingana na Uislamu kwa ujumla. Mashirika mengi ya kupigania haki za binadamu yameorodhesha mamia ya mauaji yanayofanywa chini ya kivuli cha mashauri yanayofanyika bila utafiti (simple policy). Takriban watu 52,000 wamefungwa gerezani bila kufikishwa katika vyombo vya sheria. Magazeti kadhaa yamefungiwa na mashule kadhaa kufungwa katika kipindi hiki cha miaka mitatu. Hadi sasa ugaidi unaofadhiliwa na serikali ya India unaendelea kama ilivyoonyeshwa na vyombo vya habari. Martin Sugarman aliitaja Kashmir kama kambi kubwa ya mateso kuliko zote ulimwenguni "The largest concentration camp in the world". Hivi karibuni, wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislamu walizuiwa kuhudhuria ibada Misikitini badala yake kufanyiwa magwaride ya utambuzi (identification parades) mbele ya wanajeshi walioficha nyuso zao. Katika kusherehekea siku ya taifa ya India wanajeshi hao wa serikali walianzisha operesheni ya kukamata watu holela kwa kile walichodai kuwa ni tahadhari ya kuzuia machafuko ya amani kwa siku hiyo. Pamoja na hayo, wanawake wa Kiislamu walidhalilishwa na kuwekwa vizuizini, wakati wengine wakicharazwa mijeledi na wapiganaji wa serikali. Nyumba zilichomwa moto wakati wakazi wa humo wakipata mateso kadhaa. Huko Srinagar, wapiganaji wa serikali waliwatisha Waislamu kwa kuwapiga faini kwa atayedhihirika kuhudhuria mazishi ya mashahidi. Juu ya hayo, faini kubwa kupita kiasi hutumika ili kuwanyamazisha na kuwatisha Waislamu. Hata hivyo Wakashmir wanaendelea kutafuta haki kwa gharama yoyote, wafe mashahidi (matyrdom) kama inavyodhihirishwa na harakati dhidi ya ugaidi unaofanywa na wanajeshi wa India. Kwa sasa, serikali za Pakistan na India zinafanya mazungumzo, kama kawaida agenda kubwa inahusu Kashmir. Wakati mazungumzo yanafanyika kuhusu hatma ya Kashmir, Waislamu wanaoishi humo wanaendelea kuuawa, kuteswa pamoja na kuhasiwa viungo vya miili yao. Maelfu ya watu wameachwa wakiwa hawana makazi na wengine wamekuwa wakimbizi. Wapigania uhuru wa Kashmir, wamebatizwa kuwa wao ni magaidi na kikwazo cha juhudi za kinachoitwa amani. Jihadi inayoendelea Kashmir imepunguzwa kuwa tatizo litakalopatiwa ufumbuzi na India pamoja na Pakistan. Hata hivyo, mataifa haya mawili yameonyesha wazi madhumuni yao kisiasa ya kutoijali Kashmir japo zinatofautiana kwa kiasi fulani kuhusika kwao kuongeza mateso na kurefusha vitendo hivi viovu kwa kushindwa kukomesha mauaji yanayofanywa na wanajeshi wa India. Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Kashmir unatoa taswira tofauti kuhusu India ambayo hufikirika kama eneo ambalo demokrasia inafanyika labda kuliko sehemu nyingine yoyote duniani. Hali halisi ya Kashmir inatuonyesha wazi kwamba Waislamu hawawezi kutegemea serikali za Kipagani (secular) kulinda na kutetea haki zao. Hivyo Uislamu ndio kanuni pekee kwa ukombozi wa kweli. Imefasiriwa kutoka katika gazeti la Mahjuba na Jumaa Mbaruku. |
Maoni yetu:
Unafiki si suala la wakati fulani
Historia ya harakati za ukombozi wa Kashmir Sheikh wa Wilaya Same ahimiza Waislamu kushiriki tamasha Sheikh awataka wanawake wajistiri Madrasat Al-Hujuun washerehekea
mwaka mpya
|
| An-nuur Home | Links | Islam Tanzania | Matoleo yaliyopita |