| Shairi
Simlazimishe Yesu ukombozi wa ulimwengu (jibu)
Wapagani itakidi, kwa mungu wao ibadi,
Ni kuwatoa waladi, chini ya miti na mikadi,
Zitolewe zamaradi, na kufukiza kwa udi,
Toleo za kiibadi, Ezekieli shahidi.
Kumi na sita idadi, ndiyo sura anonadi,
Ibara yake shahidi, ishirini ima zaidi,
Uangaze ushahidi, maandiko ya Wadudi,
Katu hawi mfisadi, kumukhimi wake Nabi.
Na Musa wa Tauhidi, na Yeremia Mjudi,
Manabii wa weledi, imara zao fuadi,
Wakemea ufisadi, wa kafara za waladi,
Haiwi kwa wetu Nabi, kumuasi wake Rabbi.
Kumbukumbu la Torati, kumi na nane shahidi,
Mistariye idadi, anza tisa na kuzidi,
Na Yeremia mjudi, saba ndipo taka rudi,
Thelathini na wahedi, mustari ndio budi.
Kwa kaulize Wadudi, vitabuye vinanadi,
Makafara ya waladi, ni machukizo ya kedi,
Vipi wasema Wahabi, Katenda ya ufisadi,
Kwani yake ni hududi, na mwingi wa ghufuradi.
Kama mwenzetu wanadi., upagani itikadi,
Za kuwatolea hadi, makafara ya waladi,
Miungu yao ya jadi, Zeu, Herme na Wamedi,
Simsingizie Nabi, katu si wa kuritadi.
Bali mdi kwa mjadi, muasisi itikadi,
Alofanya ukaidi, kuyapinga yalo hadi,
Na kuleta yaso budi, alotoa kwa wajadi,
Wakufuru na ya kedi, kusingizia Wadudi.
Si kejeli wala kedi, ninakupa ushahidi,
Kamrejee Luka (di), kama wewe u mweledi,
Kwenye “Matendo” anadi, “Mungu – mtu”, Mungu jadi,
Kumi na nne idadi, ibara kumi wahedi.
Kwa nini umwabe Yesu, “alofufuka” ni Zue,
Au Herme, Adonisu, idadi yao ni kuu,
Na Paulo ‘simsifu’, kwani mamboye makuu,
Amewazuga lufufu, ya chini kufanya juu.
Amechukua la Yesu, mbandikizia Zeu,
Wafilipi kaarifu, sura ya pili nukuu,
Ibara ya tano shufu, mpaka ya nane juu,
Taona uharibifu, usijedhani nafuu,
Simlazimishe Yesu, ukombozi wa “Wanguu”.
Meno,
S.L.P. 9409,
Dar es Salaam.
Utaratibu wa kupa
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Kuangukia makaa hakuna nafuu kwa aliye kikaangoni
Wanawake Dodoma wataka mtoto aliyepigwa
risasi akatibiwe nje
Kesi za Mwembechai zaanza kusikilizwa
Fitna ya Bakwata
Dondoo za saikolojia: Tuonavyo mambo
Waraka wa Baraza Kuu kuhusu Parole
Inawezekana kufanyika mdahalo kati
ya Waislamu na wasio Waislamu?
Na Nandenga wa Mkomidachi
Teknologia
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (2)
Na Hassan Omar
Serikali ihamie Dodoma kwanza !
Na. Said Rajab
Mahafali ya AMSIR Iringa
Na Mwandishi Wetu
Madrasatul Nnajjary Islamiya
Ijue Madrasatul Riyaadh
Bihawana Sekondari wafungua
Ijumaa
Vijana Shinyanga watakiwa
kuwa mfano mwema
Na Jihad R. Saballa, Shinyanga
Vyeo visiwasahaulishe majukumu
yenu- Sheikh Abri
Na Mwandishi Wetu, Iringa
Jiandaeni na kifo – Sheikh
Abdallah
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Semina zawazindua wanawake
Bukoba
Na Nadhiru Ishengoma
Waislamu wanaomaliza Kidato
cha Nne Tanga waaswa
Na Ibn Mohamed
Ndugu Kamuhabwa ndiye mwenye
chuki na AN-NUUR
Mwandishi: Maalim Bassalah
'Ukombozi wa mwanamke si kugeuzwa
biashara huria'
Na Japhary Lemah, Arusha
Polisi walinda amani katika
muhadhara wa Wakristo
Na Badru Kimwaga
Mazengo wapewa uwanja wa
kujenga Msikiti
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
'Ajiengua Chuoni Z'bar kwa
kutoruhusiwa kuvaa hijab'
Na Seif Hamad Suleiman, Zanzibar
Barua za wasomaji
Masomo ya dini ya Kiislam
Shairi
Simlazimishe Yesu ukombozi wa ulimwengu (jibu)
|