AN-NUUR 
Na.172 Rajab 1419, Oktoba 23 - 29, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Vyeo visiwasahaulishe majukumu yenu- Sheikh Abri
Na Mwandishi Wetu, Iringa

SHEIKH mmoja mashuhuri mkoani Iringa na nchini kote, Sheikh Saidi Abri; amewakumbusha wanafunzi Waislamu wajibu wao wa kuendeleza harakati za Kiislamu popote watakapokuwa pindi wakimaliza masomo yao. 

Akiongea katika hafla ya kuwaaga wanafunzi wanaomaliza masomo yao mwaka huu Sheikh Abri alisema kwamba lau wanafunzi wakishamaliza masomo yao wanayakumbuka mateso waliyoyapata kwa ajili ya dini yao wakiwa shuleni na wakasaidia kuyatatua basi wanafunzi Waislamu leo wasingenyanyasika mashuleni. Lakini akasema wengi wakishamaliza masomo huyasahau yote waliyoazimia wakiwa wanafunzi. 

Sheikh alihoji kuwa ni mara ngapi watu wamelazimishwa kwenda kuosha nguruwe na kusafisha mabanda yao hali wao ni Waislamu? Ni mara ngapi Waislamu wamenyimwa haki zao za kupata fursa ya kuabudu sawa na wasiokuwa Waislamu siku ya Ijumaa. Ni mara ngapi Waislamu wamenyanyaswa kwa ajili ya vazi la hijab na Uislamu wao kwa ujumla. "Lakini je Waislamu wangapi wanaokumbuka mateso haya wanapopata nafasi katika Serikali hii au taasisi zingine binafsi zikiwemo zile za Kiislamu kama vile Africa Muslim Agency, IIRO, World Muslim League na nyenginezo". Tumesahau yote yaliyokuwa yakitupata tukiwa shuleni au tunadhani sasa hayapo, Sheikh alihoji. 

Lakini badala yake Muislamu akipewa cheo kidogo tu hata cha utendaji wa Kata basi yeye ndiye wa kwanza atakayetoa kibali ili kilabu ya pombe ijengwe karibu na msikiti. Amesahau yote aliyoahidi akiwa AMSIR au taasisi nyingine mashuleni. 

Aliwashauri Waislamu kudumisha Tawheed ili kuwa na umoja na mshikamano, kwani hivi vyote vitakuwa ni ndoto iwapo hatutampwekesha Allah (s.w.). 

Jiandaeni na kifo – Sheikh Abdallah
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

IMAMU wa Masjid Quba Sheikh Abdallah Ally bin Ahmed amewausia mamia ya waumini wa Kiislamu waliohudhuria sala ya Ijumaa hivi karibuni kujiandaa na kifo kwa kufanya amali nzuri. 

Akitoa hutoba yake katika Masjid Quba, Sheikh Abdallah alisema kitendo cha mja kumuasi Mola wake, katu asitegemee kufaulu na kupata radhi zake hapa duniani na akhera. 

Sheikh Abdallah alisisitiza suala zima la Waislamu kurejea kwa Mola wao, kufanya amali nzuri, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya mja kupata utulivu katika moyo wake. 

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa maandalizi ya Ijtimai ya Markazi Kuu Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam, Sheikh Mtoa Mzee Mtoa akiwa hapa mjini Dodoma, alitoa nasaha zake baada ya sala ya Ijumaa katika Masjid Quba kwa kuwaelezea baadhi ya sifa nne za muumini ili aweze kufaulu. 

Akifafanua sifa hizo, Sheikh Mtoa alizitaja sifa ya kwanza kuwa ni unyenyekevu katika sala, na sala hiyo lazima imlinde mtu katika mambo maovu na machafu. 

Aidha, sala hizo zisaliwe kwa nyakati zake zimfanye awe mwenye kuyaondoa mambo maovu kwa mikono yake, ulimi au achukie uovu katika nafsi yake. 

Akitaja sifa ya pili, Sheikh Mtoa alisema muumini lazima ajiepushe na mambo ya laghwi (mambo ya upuuzi) badala yake atumie muda wake kusoma Qur’an, kutafuta riziki ya halali na kumtaja sana Allah (s.w.). 

Sifa ya tatu, Sheikh Mtoa aliwatahadharisha kwa wale wenye vipato vinavyofikia viwango vya kutoa zaka (nisabu), basi wawe wepesi kutoa zaka zao kama ambavyo wanakuwa wepesi kulipa kodi nyingine. 

Sheikh Mtoa aliwaeleza kwamba moja ya faida ya kutoa zaka ni kuifanya mali yako kuwa katika hifadhi ya Allah (s.w.). 

Akijumuisha nasaha zake, Sheikh Mtoa aliielezea sifa ya nne ya muumini kuwa ni kuhifadhi tupu zao. Alieleza kusikitishwa na tabia ya uzinifu ilivyoshamiri hali ya kuwa wazazi wa kifumbia macho vitendo hivyo. 

Semina zawazindua wanawake Bukoba
Na Nadhiru Ishengoma

SEMINA za wanawake Waislamu ambazo zimekuwa zikifanyika mara kwa mara zimetoa mchango mkubwa sana katika kuhuisha Imani na ucha Mungu kwa wanawake hao. 

Kwa mujibu wa tathmini ya matokeo ya semina hizo ufahamu wao katika Uislamu huongezeka na kumekuwa na ongezeko kubwa kwa wanawake wanaovaa hijaab. 

Semina za hivi karibu ni pamoja na ile ya mwaka jana ambayo ilihudhuriwa na washiriki wapatao 326 kutoka wilaya zote za Mkoa wa Kagera. 

Semina ya mwaka huu japo ilikuwa na washiriki wachache 158 ikilinganishwa na wale wa mwaka jana lakini imeelezwa kuwa na mafanikio makubwa zaidi kwa vile ilipata wahadhiri na washiriki toka mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza. Wenyeji wa semina hiyo walikuwa ni wanadarsa za Fauz, Migena, Nyakanyasi, Alhasanain Bilele na Forodhani. 

Kubwa lililosisitizwa katika semina hiyo ni utafutaji wa elimu na kushikana na maadili Uislamu. 

Katika risala ambayo ilisomwa mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa, Mhe. Mohamed Babu, akina mama Waislamu Bukoba waliitaka Serikali itoe waraka utakaotoa maelekezo kwa wakuu wa Idara za Serikali kwamba wasiwanyanyase wanawake wanaovaa hijab maofisini. 

Aidha, risala hiyo ambayo ilisomwa na Bi. Shura Husain iliwahimiza wazazi wote kuwashonea watoto wao wa shule za msingi na sekondari hijab kulingana na rangi zinazokubalika shuleni. 

Naye msemaji mkuu wa wanawake Waislamu mkoani Kagera Bi. Fatuma Idd Mabruk aliwaomba wanawake watayarishe vituo maulum vya uenezaji wa Da’wah na kuweka uongozi madhubuti utakaoweza kusimamia utekelezaji na kufanya tathmini. 

Waislamu wanaomaliza Kidato cha Nne Tanga waaswa

Juu 
 
YALIYOMO 
 
TAHARIRI 
Kuangukia makaa hakuna nafuu kwa aliye kikaangoni 

Wanawake Dodoma wataka mtoto aliyepigwa risasi akatibiwe nje 

Kesi za Mwembechai zaanza kusikilizwa 

Fitna ya Bakwata 

Dondoo za saikolojia: Tuonavyo mambo 

Waraka wa Baraza Kuu kuhusu Parole 

Inawezekana kufanyika mdahalo kati ya Waislamu na wasio Waislamu? 
Na Nandenga wa Mkomidachi 

Teknologia 
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (2) 
Na Hassan Omar 

Serikali ihamie Dodoma kwanza ! 
Na. Said Rajab 

Mahafali ya AMSIR Iringa 
Na Mwandishi Wetu 

Madrasatul Nnajjary Islamiya 

Ijue Madrasatul Riyaadh 

Bihawana Sekondari wafungua Ijumaa 

Vijana Shinyanga watakiwa kuwa mfano mwema 
Na Jihad R. Saballa, Shinyanga 

Vyeo visiwasahaulishe majukumu yenu- Sheikh Abri 
Na Mwandishi Wetu, Iringa 

Jiandaeni na kifo – Sheikh Abdallah 
Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

Semina zawazindua wanawake Bukoba 
Na Nadhiru Ishengoma 

Waislamu wanaomaliza Kidato cha Nne Tanga waaswa 
Na Ibn Mohamed 

Ndugu Kamuhabwa ndiye mwenye chuki na AN-NUUR 
Mwandishi: Maalim Bassalah 

'Ukombozi wa mwanamke si kugeuzwa biashara huria' 
Na Japhary Lemah, Arusha 

Polisi walinda amani katika muhadhara wa Wakristo 
Na Badru Kimwaga 

Mazengo wapewa uwanja wa kujenga Msikiti 
Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

'Ajiengua Chuoni Z'bar kwa kutoruhusiwa kuvaa hijab' 
Na Seif Hamad Suleiman, Zanzibar 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Shairi 
Simlazimishe Yesu ukombozi wa ulimwengu (jibu)  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita