AN-NUUR 
Na.172 Rajab 1419, Oktoba 23 - 29, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Wanawake Dodoma wataka mtoto aliyepigwa risasi akatibiwe nje 
 
  • Baraza Kuu laomba kibali serikalini
  • Wizara yaitupia mpira Muhimbili
WITO umetolewa kwa Waislamu na wananchi wote nchini kutoa michango yao ili kumpatia matibabu ya kufaa mwanafunzi Chuki Athumani. 

Wakiongea baada ya kongamano lao wanawake Waislamu wa mjini Dodoma wamesema itakuwa ni jambo la kushangaza wazazi kuwahangaikia watoto wao binafsi wapate elimu bora huku wakimwacha Chuki Athumani wodini kwa miezi tisa sasa. 

Walisema Chuki amedhulumiwa na ni lazima ndugu zake Waislamu na wananchi kwa ujumla wamsaidie kupata matibabu nje ya nchi ili ikiwezekana atembee kama alivyokuwa kabla ya kupigwa risasi na polisi. 

Awali katika kongamano hilo, maelfu ya wanawake hao Waislamu walilaani udhalimu waliofanyiwa Waislamu pale Mwembechai kwa kuuliwa kwa risasi za moto na wanawake kudhalilishwa. 

Wamehoji inakuwaje serikali idai ni ya uadilifu halafu ifumbie macho tendo la raia kuuliwa bila kosa tena kwa kulengwa shabaha "piga yule". 

Akiwakumbusha juu ya wajibu wao, mama Muslim aliwahimiza wanawake Waislamu kushikamana na vazi la hijaabu. Alisema mwanamke kutokuvaa hijaab anakuwa sawa na waya wa umeme usiovishwa kizuizi (insulator). 

Mama Muslim alisisitiza kwamba dawa ya ukimwi sio "mipira ya zinaa" bali kufuata sheria za Allah (sw). 

Alizitaja nchi za Waislamu kama Iran na Saudi Arabia ambapo athari ya ukimwi ni ndogo sana ikilinganishwa na sehemu nyingine duniani. 

Naye Bi. Ummy Salama aliwahimiza akina mama Waislamu washikamane katika kutafuta elimu, kujua haki zao, sheria na kuyajua mazingira yao kwa ujumla ili waweze kuifanya kazi ya Da’wah kwa ukamilifu. 

Ummy Salama aliwaonya vikali wanawake Waislamu wanaotafuta suluhisho la matatizo yao kwa kufuata kanuni za kitwaghuti. Aliwahimiza waisome Qur’an na waangalie masuala ya ndoa, talaka na mirathi. 

Kongamano hilo la wanawake Waislamu mjini Dodoma liliandaliwa na kikundi cha akina mama wa Kiislamu cha Bi. Khadija na kufanyika katika shule ya Al-Hijrah Oktoba 17, 1998. 

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu amesema kwamba tayari Baraza limemuandikia Waziri wa Afya Mh. Aron Chiduo ili atoe taratibu za kufuatwa na gharama za kumtibia mwanafunzi Chuki Athumani nchi za nje. 

Sheikh Kilima alisema kwamba kinachotakiwa ni mtoto Chuki kufanyiwa upasuaji na wataalamu wa mishipa ya fahamu (Neural Surgions) kwa tegemeo la kumuondolea kilema cha kulemaa. 

Aliwataka Waislamu na wananchi kwa ujumla kuwa tayari kutoa sadaka zao kumsaidia mtoto Chuki pindi Mh. Waziri atakapotoa gharama zinazohitajika. 

Hata hivyo taarifa ambazo AN-NUUR imezipata baadaye zimeeleza kwamba Wizara ya Afya kupitia barua yake No. HEC 426 ya Oktoba 22, 1998 imelielekeza Baraza Kuu kufuatilia taratibu za mtoto Chuki kutibiwa nje ya nchi huko huko Muhimbili. 

Haikuweza kufahamika mara moja ni kwanini Wizara ya Afya imechukua muda mrefu kiasi hicho kutoa maelekezo hayo. 

Maombi ya Baraza Kuu yalipelekwa kwa Mh. Waziri Chiduo tangu Julai 2, 1998. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
TAHARIRI 
Kuangukia makaa hakuna nafuu kwa aliye kikaangoni 

Wanawake Dodoma wataka mtoto aliyepigwa risasi akatibiwe nje 

Kesi za Mwembechai zaanza kusikilizwa 

Fitna ya Bakwata 

Dondoo za saikolojia: Tuonavyo mambo 

Waraka wa Baraza Kuu kuhusu Parole 

Inawezekana kufanyika mdahalo kati ya Waislamu na wasio Waislamu? 
Na Nandenga wa Mkomidachi 

Teknologia 
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (2) 
Na Hassan Omar 

Serikali ihamie Dodoma kwanza ! 
Na. Said Rajab 

Mahafali ya AMSIR Iringa 
Na Mwandishi Wetu 

Madrasatul Nnajjary Islamiya 

Ijue Madrasatul Riyaadh 

Bihawana Sekondari wafungua Ijumaa 

Vijana Shinyanga watakiwa kuwa mfano mwema 
Na Jihad R. Saballa, Shinyanga 

Vyeo visiwasahaulishe majukumu yenu- Sheikh Abri 
Na Mwandishi Wetu, Iringa 

Jiandaeni na kifo – Sheikh Abdallah 
Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

Semina zawazindua wanawake Bukoba 
Na Nadhiru Ishengoma 

Waislamu wanaomaliza Kidato cha Nne Tanga waaswa 
Na Ibn Mohamed 

Ndugu Kamuhabwa ndiye mwenye chuki na AN-NUUR 
Mwandishi: Maalim Bassalah 

'Ukombozi wa mwanamke si kugeuzwa biashara huria' 
Na Japhary Lemah, Arusha 

Polisi walinda amani katika muhadhara wa Wakristo 
Na Badru Kimwaga 

Mazengo wapewa uwanja wa kujenga Msikiti 
Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

'Ajiengua Chuoni Z'bar kwa kutoruhusiwa kuvaa hijab' 
Na Seif Hamad Suleiman, Zanzibar 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Shairi 
Simlazimishe Yesu ukombozi wa ulimwengu (jibu) 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita