|
|
| Mafundisho
ya Qur'an
Kuwepo kwa ufufuo Aya ya 259 "AU kama yule aliyepita karibu na mji uliokuwa umekufa aksema: "Allah atauhuiisha vipi mji huu baada ya kufa kwake?" Basi Allah alimfisha kwa miaka mia, kisha akamfufua akamuuliza: "Umekaa muda gani? Akasema: Nimekaa muda wa siku moja au sehemu ya siku". Allah akasema: "Bali umekaa miaka mia, nawe tazama chakula chako na kinywaji chako havikuaribika. Na mtazame punda wako. Na ili tukufanye uwe hoja kwa watu. Na itizame mifupa ya punda wako jinsi tunavyoinyanyua kisha tunaivisha nyama". Basi yalipobainika alinena: "Najua kwamba Allah ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu" Aya hii inhali ni mlolongo wa aya iliyotangulia na nyingine baada ya kumkubali. Kwa kweli si rahisi kumtaja mtu huyu alikuwa nani au aliishi wakati wa zama zipi na mji huu unaoelezwa hapa ni mji gani. Tunachojifunza katika aya hii ambayo ni moja ya ushahidi wa kuwepo ufufuo ni namna gani Allah anavyowaongoza wale wanaomuamini na wakampiga vita Twaghut. Kinachoonekana hapa ni kuwa mtu huyu inawezekana kuwa alikuwa na imani yake kwa Allah lakini alikuwa hajatulia kwenye imani hiyo na hivyo Allah akachukua nafasi ya suala lake hilo kumuonyesha kwa vielelezo hai suala hilo na uwezekano wa kutokea kwake kuwa ni wa hakika na siyo kubahatisha. Hali ya mji ilivyokuwa, kwamba huko nyuma mji huo ulikuwa na watu wanaoishi na harakati za kila namna lakini wakati huo ulikuwa ni kihame na masalia ya magofu. Picha hiyo ilimpelekea kujiuliza kuhusu maisha baada ya kufa kwani mji huo ulikuwa ni sawa na mfu (maiti). Jawabu la Allah ni kumfisha kwa miaka mia moja au karne nzima kwa lugha nyingine. Kama kawaida ya umri wa binadamu na maisha ya binadamu, siku zote umri hamna kitu na ndiyo maana mtu huyu akaona kuwa amelala hapo kwa siku mja au kasoro. Hali hii inaonekana hata kwa watu wengine siku ya kiyama au baada ya hapo. Hebu tujikumbushe baadhi ya aya zinazoonyesha mfano wa mtu huyu siku ya kiyama: "Basi litakapopulizwa parapanda, hapo hautakuwepo ujamaa baina yao siku hiyo wala hawataulizana. Ama wale ambao mizani yao itakuwa nyepesi, nao ndio waliozitia hasarani nafsi zao, na katika Jahanamu watakaa milele. Atawauliza Allah: "Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hesabu ya miaka?" Watasema: "Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wafanyao hesabu. (23:101, 102, 112 - 113). "Wanakuuliza kiyama kutokea kwake kutakuwa lini? Uko wapi na kuweza kutaja (wakati wa kuja Kiyama)? Mwisho (wa ujuzi) wake uko kwa Mola wako. siku watakapokiona watakuwa kana kwamb hawakukaa (ulimwenguni) ila jioni moja au mchana wake. (79:42-46). Karne moja kwa mtu ni kipindi kikubwa ingawaje kwa Allah ni muda mdogo sana kwani yeye hana mwanzo wala hana mwisho. Mtu huyu alipotea yeye binafsi na punda wake lakini Allah kwa uwezo wake alihifadhi chakula na kinywaji chake. Kikawaida chakula ndicho chepesi kuharibika kuliko binadamu wakati kinywaji ni chepesi kupotea ama kwa sababu ya jua au upepo. Kwa kuwa lengo ni kutoa funzo, Allah alivihifadhi viel vyepesi kuharibika na akaviacha viteketee vile vinavyohisikana kuwa ni vigumu (kama binadamu na punda). Wa kwanza kuamshwa kwa ufufuo alikuwa huyu binadamu ili ashuhudie uwezo wa Allah kwa macho yake. Kwa amri yake Allah aliipanga mifupa mibovu na kuivika nyama mbele yake na mara punda akawa punda kwa kutembea na kulia. Chakula ambacho hakikuonekana na ulinzi kilibaki kizima pasipo na dosari. Mtu huyu baada ya kupambanukiwa na ukweli wa mambo pale pale alisema kwa kuyakinisha kabisa kuwa Allah ana uwezo juu ya kila kitu. Picha hii ni tofauti na ile ya Namrudh ambaye alipopambanukiwa na haki yeye alisimama kidete kuikanusha kwa kibri na akaendelea kuwalazimisha wengine kumuabudu yeye badala ya Mola wake. "Na (kumbuka) Ibrahimu aliposema: "Mola wangu! Nionyeshe jinsi utakavyofufua wafu". Allah akasema: "Huamini?" Akasema: "La, naamini, lakini nataka moyo wangu utulie (zaidi)". Akasema Allah: "Basi chukua ndege wanne na uwazoeshe kwako, kisha (wachinje) na uwaweke juu ya kila jabali sehemu katika wao. Kisha waite, watakuja mbio. Na ujue ya kwamba Allah ni Mwenye nguvu na Mwenye Hikima". Aya hii bado ingali katika mtiririko wa kutoa mifano ya watu ambao Allah anawaongoza pamoja na kuonyesha uwezo wake. Kikubwa zaidi ambacho tunakisoma katika aya hii ni uthibitisho wa waziwazi na usio na shaka kuhusiana na kuwepo ufufuo baada ya kufa kwa viumbe. Kama aya inavyoeleza, si dalili ya kutokuamini kwa Nabii Ibrahimu (as) kutaka aonyeshwe namna Allah anavyofufua, bali ni kutaka utulivu na yakini ambayo hupatikana kwa elimu ya yakini na hali halisi ya mambo ilivyo. Ni kwa sababu hiyo ndiyo Allah hakumlaumu Nabii wake na badala yake akafanya kama alivyotaka Nabii wake huyo. |
YALIYOMO
TAHARIRI Hakuna Muislamu aliyekufa kutokana na vurugu Mgogoro wa kiwanja Duma: Wakatoliki wasema kuna njama za Waarabu Same Na Mwandishi Wetu Wanawake wakutana Mwanza na kusema: Kunyanyaswa sasa basi Na Mwandishi Wetu, Mwanza Sheikh Omar Bashir ataka Waislamu waimarishe mshikamano Na Said Sharif Ustaadhi Abdallah Mfoyi afariki Na Muhibu Saidi Baraza Kuu halina Katibu Nguruka - Sheikh Kilima Na Abu Adli Viongozi Msikiti wa Ubungo Darajani waitwa polisi Na Kassim Juma Marekani `ilivyosaidia' Mujahidiin Barua ya mtoto wa miaka minne toka Lebanon kwa Bibi Hillary Clinton Ujumbe wa waandishi kwa Bw. Batendi, Wakristo Na Muhibu Saidi Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha Tusiwe Jogoo wa Esopo na Almasi Na MAALIM ALI BASSALEH Sherehe za wiki ya usalama barabarani: Kauli nzito za waheshimiwa zimekalia kuti kavu Na Said Omar Mwanasayansi Avicenna: Tabibu bingwa. Na Dk. A. A. Amur Ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa Mriti waanza Na Nasib A. Mziray Kutoweka kwa hazina adimu za kimazingira Na Yassir Salim Mfalme Najashi ni mfano bora wa kuigwa kwa watawala Na Idi Kikong'ona Waislamu Moro wasaidia wagonjwa Na Mwandishi Wetu, Morogoro KUFUATIA KUTISHIA MAGAZETI: Sheikh Ayoub amjibu Askofu Rajab Rajab Na Mussa Ally TAMSA Tanga waahidi kuendeleza mema Na Ibn Mohammed, Tanga Ufugaji, uuzaji nguruwe wakera wananchi Dar Na Mwandishi Wetu Mafundisho ya Quran Kuwepo kwa ufufuo Barua za wasomaji
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org