|
|
| Wanawake
wakutana Mwanza na kusema:
Kunyanyaswa sasa basi
Na Mwandishi Wetu, Mwanza' WANAWAKE Waislamu waliokutana mjini Mwanza hivi karibuni wameungana na Waislamu wenzao kote nchini kuitaka serikali iwachukulie hatua waliohusika na mauaji ya Waislamu pale Mwembechai. Wakihitimisha kongamano lao la siku moja, akina mama hao waliofurika katika Ukumbi wa Thaqaafa, waliitaka serikali ifanye kazi zake kwa uadilifu na sio kusema haina dini huku inaonyesha kwa uwazi kufanya upendeleo kwa misingi ya dini. Wanawake hao waliwataka wanawake kote nchini watafakari nini wamejifunza na nini cha kufanya baada ya tukio la Mwembechai. Aidha, wamewataka watafakari kwanini serikali imeridhia tendo la wanawake Waislamu kuvuliwa nguo na kupekuliwa na polisi wanaume wakati askari polisi na wale wa Magereza wapo wanawake. Ni upi unyanyasaji na udhalilishaji wa wanawake; wamehoji. Kongamano hilo la aina yake mkoani Mwanza, lilifunguliwa kwa Qur'an tukufu iliyosomwa na Halima Issa ikifuatiwa na dua iliyosomwa na Hadija Omar. Akina mama hao wapatao elfu moja na zaidi walijikuta wakiangua kilio pale walipokumbushwa mateso na vitendo vya kinyama walivyofanyiwa na polisi wanawake wenzao Msikitini Mwembechai na huko gerezani. Katika kongamano hilo mabinti wawili walisilimu ambao ni Justina Emmanuel (Anglikana) ambaye alichagua jina la Mwanaidi na Upendo Nicholaus (Mkatoliki) aliyechagua jina la Fatma. |
YALIYOMO
TAHARIRI Hakuna Muislamu aliyekufa kutokana na vurugu Mgogoro wa kiwanja Duma: Wakatoliki wasema kuna njama za Waarabu Same Na Mwandishi Wetu Wanawake wakutana Mwanza na kusema: Kunyanyaswa sasa basi Na Mwandishi Wetu, Mwanza Sheikh Omar Bashir ataka Waislamu waimarishe mshikamano Na Said Sharif Ustaadhi Abdallah Mfoyi afariki Na Muhibu Saidi Baraza Kuu halina Katibu Nguruka - Sheikh Kilima Na Abu Adli Viongozi Msikiti wa Ubungo Darajani waitwa polisi Na Kassim Juma Marekani `ilivyosaidia' Mujahidiin Barua ya mtoto wa miaka minne toka Lebanon kwa Bibi Hillary Clinton Ujumbe wa waandishi kwa Bw. Batendi, Wakristo Na Muhibu Saidi Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha Tusiwe Jogoo wa Esopo na Almasi Na MAALIM ALI BASSALEH Sherehe za wiki ya usalama barabarani: Kauli nzito za waheshimiwa zimekalia kuti kavu Na Said Omar Mwanasayansi Avicenna: Tabibu bingwa. Na Dk. A. A. Amur Ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa Mriti waanza Na Nasib A. Mziray Kutoweka kwa hazina adimu za kimazingira Na Yassir Salim Mfalme Najashi ni mfano bora wa kuigwa kwa watawala Na Idi Kikong'ona Waislamu Moro wasaidia wagonjwa Na Mwandishi Wetu, Morogoro KUFUATIA KUTISHIA MAGAZETI: Sheikh Ayoub amjibu Askofu Rajab Rajab Na Mussa Ally TAMSA Tanga waahidi kuendeleza mema Na Ibn Mohammed, Tanga Ufugaji, uuzaji nguruwe wakera wananchi Dar Na Mwandishi Wetu Mafundisho ya Quran Kuwepo kwa ufufuo Barua za wasomaji
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org