|
|
| Mgogoro wa
kiwanja Duma:
Wakatoliki wasema kuna njama za Waarabu Same
Na Mwandishi Wetu HABARI kutoka Duma wilayani Same zimeeleza kwamba Wakatoliki wamepinga hukumu ya mahakama ya mwanzo iliyowapa ushindi Waislamu katika Shauri la Madai No. 63/98. Katika kupinga kwao hukumu hiyo Wakatoliki wamedai kwamba wana ushahidi kwamba Waislamu wamepatiwa fedha kutoka Iran, Iraq, Somalia na Zanzibar. Aidha, wameitaka mahakama ilipe uzito dai lao la kutengua ushindi wa Waislamu kwa madai kwamba tayari eneo hilo linatembelewa na Waarabu. Wamedai kwamba kuja kwa Waarabu hao kumewapa wasiwasi Wakatoliki kwamba huenda Waarabu wanayo njama fulani huko Duma. Pamoja na maelezo hayo, habari kutoka Duma zimeeleza kwamba Wakatoliki katika moja ya sababu zao za kukata rufaa, wamedai kwamba Waislamu wamewatishia kuwahamisha kwa vile wanafuga nguruwe. Waislamu walitakiwa na mahakama ya wilaya kwamba wawe wameshajibu hoja hizo za Wakatoliki pamoja na nyingine zilizowasilishwa mahakamani Septemba 1I, mwaka huu. Hata hivyo, Waislamu wameiomba mahakama hiyo iwape muda zaidi na sasa Shauri litatajwa Oktoba 2, 1998. Katika Shauri hilo, Waislamu walidai kwamba Wakatoliki walikuwa wamevamia eneo lao la Msikiti na shule walilopewa toka mwaka 1953. Julai 30, mwaka huu mahakama ya mwanzo Same ilitoa hukumu kwamba eneo linalolalamikiwa ni la Waislamu na Wakatoliki waliamriwa kulipa fidia ya miti waliyokata. |
YALIYOMO
TAHARIRI Hakuna Muislamu aliyekufa kutokana na vurugu Mgogoro wa kiwanja Duma: Wakatoliki wasema kuna njama za Waarabu Same Na Mwandishi Wetu Wanawake wakutana Mwanza na kusema: Kunyanyaswa sasa basi Na Mwandishi Wetu, Mwanza Sheikh Omar Bashir ataka Waislamu waimarishe mshikamano Na Said Sharif Ustaadhi Abdallah Mfoyi afariki Na Muhibu Saidi Baraza Kuu halina Katibu Nguruka - Sheikh Kilima Na Abu Adli Viongozi Msikiti wa Ubungo Darajani waitwa polisi Na Kassim Juma Marekani `ilivyosaidia' Mujahidiin Barua ya mtoto wa miaka minne toka Lebanon kwa Bibi Hillary Clinton Ujumbe wa waandishi kwa Bw. Batendi, Wakristo Na Muhibu Saidi Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha Tusiwe Jogoo wa Esopo na Almasi Na MAALIM ALI BASSALEH Sherehe za wiki ya usalama barabarani: Kauli nzito za waheshimiwa zimekalia kuti kavu Na Said Omar Mwanasayansi Avicenna: Tabibu bingwa. Na Dk. A. A. Amur Ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa Mriti waanza Na Nasib A. Mziray Kutoweka kwa hazina adimu za kimazingira Na Yassir Salim Mfalme Najashi ni mfano bora wa kuigwa kwa watawala Na Idi Kikong'ona Waislamu Moro wasaidia wagonjwa Na Mwandishi Wetu, Morogoro KUFUATIA KUTISHIA MAGAZETI: Sheikh Ayoub amjibu Askofu Rajab Rajab Na Mussa Ally TAMSA Tanga waahidi kuendeleza mema Na Ibn Mohammed, Tanga Ufugaji, uuzaji nguruwe wakera wananchi Dar Na Mwandishi Wetu Mafundisho ya Quran Kuwepo kwa ufufuo Barua za wasomaji
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org