|
Na. 071 Jumatano Oktoba 25 - 31, 2000 |
|
|
|
|
|
Na Mwandishi Wetu WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani wameazimia kuendelea na mgomo wa kutoingia darasani leo hadi hapo madai yao yatakapotekelezwa. Wakiongea na Afisa Utawala wa chuo hicho, Prof. Mkude ambaye alitoa tamko la Baraza la Chuo lililowataka wanafunzi wasimamishe mkutano wao na kurejea madarasani, wamesema wataendelea na msimamo wao mpaka pale matatizo yao yatakapotatuliwa. Mgomo huo wa wanafunzi ulianza Jumatatu Oktoba 23 ambapo wasomi hao walikuwa wakijadili masuala mbalimbali yanayohusu madai yao katika baraza la wanafunzi badala ya kuingia darasani. Madai ya wanafunzi hao ni kuongezewa fedha kwa ajili ya chakula na malazi kutoka Shs.2000 hadi shs. 3,500 kwa siku, fedha za vitabu kutoka shs. 100,000 hadi Shs.150,000 na posho ya usafiri kwa wanafunzi wanaokaa nje ya chuo hicho,kwa vile viwango vya sasa ni vidogo kulinganisha na halisi ya maisha. Pia wanafunzi hao wameutaka uongozi wa chuo hicho kuwarudisha wenzao waliopewa barua za kusimamishwa masomo kuanzia jana. Msimamo wa wanafunzi hao kuendelea na mgomo wao umekuja wakati Baraza la Chuo Kikuu hicho limetoa taarifa inayowaagiza wanafunzi hao kurudi darasani mara moja. Katika taarifa hiyo ya Oktoba 24 mwaka huu iliyotiwa saini na Kaimu Makamu mkuu wa chuo kikuu hicho cha kwanza nchini, Prof. M. H. H. Nkunya, Baraza hilo limesema wanafunzi wote waliogoma siku ya tarehe 23 na 24 mwezi huu tayari wamekiuka sheria za chuo hicho na watashughulikiwa ipasavyo, na kuongeza kwamba iwapo wataendelea na mgomo hatua zaidi zitachukuliwa dhidi yao. Jumamosi Oktoba 21 mwaka huu mvutano kati ya wanafunzi hao na serikali ulipelekea wanafunzi hao kumzuia Waziri Mkuu, Mhe. Fredrick Sumaye kufanya mkutano wa katika kiwanja muhimu chuoni hapo, Revolutionary Square, kwa madai kuwa "kiwanja hicho ni eneo takatifu na hakiwezi kutumiwa na watu ambao wameshindwa kupambana na rushwa". Msimamo huo wa wanafunzi ulimlazimisha Mhe. Sumaye
kuhamishia mkutano wa katika viwanja vya shule ya Msingi mlimani iliyopo
ndai ya eneo la chuo kikuu hicho. Hata hivyo wanafunzi hao hawakudhuria.
Kadinali Pengo aliyasema hayo katika ibada ya kuombea amani uchaguzi mkuu ujao. Ibada hiyo iliandaliwa na umoja wa wanawake wakikatoliki mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Hivi karibuni kumekuwepo malalamiko mengi toka kwa wananchi na vyama vya upinzani kuhusu wasiwasi wa kuwepo wezi wa kura katika uchaguzi mkuu ujao. Mwanzoni mwa mwezi huu wafuasi wa vyama kadhaa vya upinzani mjini Mwanza waliwakamata watu waliodaiwa kukutwa na vitabu vya shaahada na baadhi ya vifaa vya kupigia kura. Miongoni mwao walidaiwa kuwepo baadhi ya watumishi wa kata, tume ya uchaguzi na chama tawala. Baadhi ya watuhumiwa hao walifikishwa kituo cha polisi lakini gazeti hili halina habari ni hatua zipi zilizochukuliwa. Pamoja na tukio hilo, Kaimu Katibu wa chama cha CUF Bw. Shaibu Akwilombe alilieleza NASAHA kuwa chama chake kiliandika malalamiko kadhaa kwa tume ya uchaguzi kuelezea wasiwasi wa chama hicho kuwepo kwa njama za wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uchaguzi mkuu ujao. Katika moja ya malalamiko yake, CUF ilieleza wasiwasi wake wa idadi ya kura zilizotangazwa na tume kuwa ni kubwa kwa kiasi cha milioni tatu ya kiasi kilichoratibiwa na chama hicho. "Wasitengeneze karatasi za kupigia kura za ziada kwani idadi ya waliojiandikisha kupiga kura ndio inayotakiwa kupiga kura Oktoba 29," alionya Kadinali Pengo. Chama hicho pia kilionesha wasiwasi wake kuhusu utata wa takwimu za idadi ya jumla ya kura zilitolewa na Tume ya uchaguzi kwa mikoa kadhaa, ikiwemo mikoa ya Rukwa, Arusha na baadhi ya majimbo ya Zanzibar na Pemba. Aidha hivi karibuni iliripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwepo kwa matukio kadhaa ya kutia wasiwasi wa kuwepo kwa kura za wizi au wizi wa kura. Matukio hayo ni pamoja na kuwepo na masanduku ya ziada ya kupigia kura katika baadhi ya mikoa kuliko idadi halisi iliyokusudiwa. Madai mengine katika matukio hayo ni pamoja na upotevu wa baadhi ya mwasanduku hayo na mengine kati yao yakihofiwa yakiwa yamejazwa kura zilizokwisha pigwa kabla ya siku ya uchaguzi. "Kuna watu ambao wanapitapita wakitengeneza karatasi za kupigia kura na kuziweka katika masanduku... hapo Mwenyezi Mungu hakuheshimiwa," alisema Kadinali Pengo. Awali chama cha wananchi CUF, ambacho mwenyekiti wake Prof. Lipumba mgombea Urais anaelekea kuungwa mkono na wananchi wengi, kilionya kwamba Watanzania wapenda demokrasia na haki nchini hawako tayari kuona kura zao zinaibiwa na waroho wa madaraka. Viongozi, wafuasi wa chama hicho pamoja na wananchi wapenda haki wamekuwa wakiwaonya wezi wa kura katika uchaguzi ujao kwamba watashughulikiwa ipasavyo. Msimamo huo wa kutetea haki umepewa jina la 'jino kwa jino." "Wale wanaogopa jino kwa jino, waache kuiba kura," wamekuwa wakionya wananchi wapenda haki, kuhusu kelele za baadhi ya watu ambao wamekuwa wakishutumu sera hiyo.
Taarifa ya kituo cha haki haikuzingatia haki
Na Mwandishi Wetu
IMEELEZWA kuwa taarifa iliyotolewa na kituo cha haki za binadamu nchini kuhusu uchaguzi mkuu ujao na kutangazwa kwenye vyombo vya habari mwishoni mwa wiki iliyopita, haikuzingatia misingi ya haki inayotarajiwa katika uchaguzi wa kidemokrasia. Hayo yameelezwa na wananchi kadhaa jijini katika maoni yao kufuatia kutolewa kwa taarifa hiyo. Katika taarifa ya kituo hicho kijulikanacho kwa Kiingereza: Legal and Human Rights Centre ambayo ilitolewa na kutangazwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini, ilieleza kuwa kituo hicho kimesikitishwa na madai ya kuwepo maneno ya vitisho ya kuwaonya wezi wa kura. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya kituo hicho iliyosomwa na Helen Kijo - Bisimba, kituo hicho kilinukuu taarifa za madai ya kuwepo vitisho vya baadhi ya vyama vya upinzani kwa wezi wa kura. Hata hivyo, katika maoni yao, wananchi hao wameeleza kwamba maneno yaliyodaiwa kuwa ni ya vitisho yalitolewa katika majukwaa ya kisiasa na yalikwisha fafanuliwa na kueleweka na wananchi; na hivyo walisikitishwa kuona kituo hicho wanaendelea kulishikilia neno kinyume na linavyoeleweka na wananchi. Wananchi hao walishindwa kuelewa ni vipi kituo hicho kikumbuke maneno yaliyosemwa na vyama vya upinzani, hasa chama cha CUF, lakini kisikumbuke yale yaliyosemwa na chama tawala. "John Malecela, Makamu Mwenyekiti wa CCM alitangaza 'mtu kwa mtu' na vyombo vya habari viliandika, ina maana hawa viongozi wa kituo hicho hawakumsikia au kusoma kwenye magazeti yaliyoandika?" alisema Bw. Mzuzuri wa Mtoni,jijini Dar es Salaam. "Bila shaka hawa viongozi wa kituo hicho ni wakereketwa wa CCM au maadui wa CUF au maadui wa watu wa Zanzibar; mbona hawakuzungumzia kauli ya Dr. Omar Ali Juma aliyosema silaha (na vifaru vya jeshi) vilipelekwa Zanzibar kwa ajili ya CUF. Na wananchi kadhaa wameshapigwa risasi Zanzibar," alisema Bw. Marcel wa Sinza. "Watu wasio zingatia na kujali haki ya pande zote, hawana haki wala hadhi ya kuleta haki," alisema Zablon wa Manzese jijini. Bi Amina wa Upanga Dar es Salaam alisema kuwa hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa kituo hicho kuonesha upendeleo. Bi Amina ambae ni mfanyakazi katika moja ya hospitali binafsi jijini Dar es Salaam alisema kuwa katika taarifa yake ya haki za binadamu: Right to life - newspapers survey: January 1997 -December 1999 ambayo ilionesha matukio kadhaa ya uvunjaji wa haki za binadamu nchini, kituo hicho kilionesha mtazamo wake wa kutokujali baadhi ya matukio hata pale ambapo binadamu wanauawa kwa kupigwa risasi. Aidha Bi Amina alisema kwamba mtazamo huo unaelekea na kupatana ule wa serikali. Alitoa mfano wa taarifa hiyo ambayo ilikusanya matukio karibu yote ya binadamu kuumizwa, kuonewa, n.k. kwa njia mbalimbali, kwa kupitia taarifa za magazeti kati ya Januari 1997 na Desemba 1999. Lakini, alisema Bi Amina kituo hicho "hakikuona" wala kujali kutaka kuona tukio la binadamu kuuawa na polisi pale Mwembechai, Dar es Salaam Februari 13, 1998, licha ya kuandikwa katika magazeti mengi ndani na nje ya nchi. "Pengine kwa mtazamo wao, Muislam si binadamu; maana waliouawa Mwembechai ni Waislamu," alisema Bi Amina na kuongeza, "hawa hawawezi kuwa na sifa ya kusikilizwa au kueleweka na jamii inayotambua usawa wa haki mbele ya binadamu." Wakati huo huo, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Duniani (Amnesty International) limezitaka taasisi na waangalizi wa Kimataifa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuchunguza kwa makini vitendo vya uvunjaji haki za binadamu ambavyo vinafanyika huko Tanzania Visiwani. Shirika hilo limesema, linasikitishwa na vitendo
vya unyanyasaji na kuteswa kwa wanachama wa chama cha upinzani wa CUF lililodai
vinafanywa na serikali.
|
YALIYOMO
Tahariri
'Mdahalo' umekwisha: CCM haikujibu hoja za Lipumba Wananchi kuhakikisha haki inatendeka Wanafunzi Chuo Kikuu kuendelea na mgomo |
|
|
|
|