NASAHA
Na. 035 Jumatano Februari 16 - 22, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Barua/Maoni



Kuraghbu umwagaji damu kunavunja hadhi; kumwaga damu je?

Ndugu Mhariri,

NAOMBA nafasi kwenye gazeti lako ili niufahamishe umma wa wapenda amani, haki na uadilifu hapa Tanzania. Kutokana na propaganda chafu zinazopandikizwa na waandishi wasiojali taaluma zao na ambao wako tayari kupotosha au kuharibu jema lolote ambalo wao hawana maslahi nalo japo litakuwa na faida na maslahi kwa walio wengi. 

Katika gazeti moja litolewalo kwa lugha ya Kiswahili kila siku la Februari 2, 2000 mwandishi mkongwe wa gazeti hilo alitoa makala yake katika ukurasa wa saba(7) yenye kusomeka "Seif, Maghimbi wajivunjia hadhi kuraghbu umwagaji damu." Kufuatia kauli zao kuhusu uchaguzi ujao kuwa hawatakubali kudhulumiwa au kufanyiwa faulo kama ile ya mwaka 1995. Mwandishi anadai eti ana hakika kauli ile ambayo ilitolewa kwa pamoja na vyama vya CHADEMA, CUF na UDP. 

Yeye anadai CHADEMA na UDP waliburuzwa na kwamba ile ni kauli ya CUF. Je anataka kutufahamisha kuwa viongozi wa UDP na CHADEMA ni mambumbumbu wasiojua kitu hata kufikia kuburuzwa? Hizi ni propaganda chafu dhidi ya CUF na viongozi wake ambazo lengo lake ni kutaka kuwavunjia hadhi na heshima mbele ya umma wa Watanzania kwa kuwa sasa CUF imekuwa tishio kwa chama tawala hivyo wapiga debe kama mwandishi huyo wanatafuta jinsi gani ya kubadili mwelekeo wa tufani dhidi yao. 

Sisi wapenda amani na haki hatutishwi na kauli hizo bali tunatishwa na vitendo vilivyofanywa Mwembechai vya watu kuuawa kisha Waziri Mkuu na Wabunge kuwapongeza wauaji na baya zaidi Mhe.Rais kudai waliouawa Mwembe Chai ni wahuni hili ndilo linalotisha zaidi nakutia simanzi nyonyo za wapenda amani wote duniani. 

Je mbwa immigaration ana THAMANI KUBWA KUZIDI WANAODAIWA KUWA WAHUNI (Waislam) wa Mwembe Chai. Je ufumbizi wa uhuni ni kuwatwanga risasi? Na je wahuni wangapi wameuawa toka zoezi hilo lianze? 

Mbona wale wahuni aliowaita hayati Mwalimu Nyerere hawakupigwa risasi? Kauli za kina Maalim Seif ni sahihi kabisa hawakukosea kwanini wakubali dhuluma eti kisa damu itamwagika amani itatoweka? Wadhulumiwa wanaamua kuondoa dhuluma kwa njia ya amani(kura) dhwalimu hataki vipi isitumike njia nyingine muafaka ili kuondoa udhia huo? 

Hata tuhuma za udini wanazo tuhumiwa CUF siyo za kweli hata kidogo na hili yeye mwenyewe anakiri hilo halipo. Kilichokuweko ni propangada za CCM dhidi yaCUF ili kisikubalike, propaganda ambazo zilipigiwa mbiu pia na magazeti na waandishi kama huyu na mfano wake. 

Udini ulioko CCM hausemwi hata kidogo. Mathalan kilichotokea mwaka 1995 dhidi ya Jakaya Kikwete wakati wa kupitisha jina la mgombea urais kwa tikiti ya CCM ni mizengwe illyotokana na dini yake au yale yaliyokuwa yakimkabili Marehemu Kigoma Malima ndani ya CCM yalikuwa ni matokeo dhahiri ya udini uliofichikana ndani ya CCM. Kauli za maaskofu dhidi ya serikali ya Alhaji Mwinyi na jinsi magazeti yalivyokuwa yakimtusi na kumkashifu pia ni udini. 

Leo hii magazeti yamepiga kimya kizito hata Mhe.Cheyo ameyauliza mbona kimya, hawasemi kitu kashfa ya Mama Mkapa kukopa pesa za NBC? Tuwe macho na waandishi mfano wa huyu ambao sio waadilifu katika taaluma yao ili mradi wako tayari kupotosha umma kwa maslahi yao binafsi. 

Mpenda amani, haki na uadilifu, 

Makinga Bundaza,
MEATU- Shinyanga.


Vizuizi vya barabarani vipo kinyume cha sheria 

Ndugu Mhariri,

TAFADHALI naomba angalau uniweke pembeni mwa gazeti lako tukufu, ili nitoe yangu yanayonikera. Hotuba ya Mheshimiwa Stephin Mwashisanga huko Shinyanga ilinisisimua mno pale alipotoboa wazi kwamba, vizuizi vyote vilivyowekwa barabarani ni kinyume cha SHERIA. Na akataka haraka viondolewe. 

Kama wananchi wa Shinyanga walivyo mwelezea mkuu wao bugudha na kero zinazofanyika kwenye vizuizi hivi, hakika havielezeki. Hapa Lindi vizuizi kama hivyo vimetapakaa kila njia. 

Watu wengi waliitikia mwito wa serekali wa kilimo, na kilimo chenye ardhi nzuri na yenye mabonde mazuri yapo Lindi vijijini. Vimewekwa vizuizi hivi, sasa imekuwa mashaka matupu. 

Ukiisha vuna chakula chako kama mahindi, mtama au mpunga, basi ufahamu kwamba umechokoza majanga. Kupeleka chakula hicho nyumbani kwako Lindi, mjini inabidi ujiandae vizuri. Kwanza ulipie ushuru wa kijiji kilichokupatia sehemu ya kulima, pili ulipie nauli ya usafirishaji, na tatu ushuru kizuizini. 

Kama huna pesa za ushuru, chakula chako chote kitateremshwa hata kama yalikuwa magunia 40. Au vinginevyo uyatoe mhanga magunia matano kama ushuru wake. Hapo kila kinachopita lazima kilipiwe ushuru. Ndiyo sehemu rushwa imekithiri. 

Vizuizi hivi vimekuwa sasa vitega uchumi vya watu wachache, si kwa maslahi ya umma. Kama kweli madhumuni yake ilikuwa kuwanufaisha wananchi, kazi yake ingalionekana. 

Imekuwa sawa na kodi ya maendeleo, iliyogeuka kuwa maendeleo ya wachache badala ya Taifa lote. 

Kama alivyobaini Mheshimiwa Mwachisanga kwamba vizuizi hivi ni uvunjaji wa sheria, basi pana haja ya wale wote walioruhusu vizuizi hivi wachukuliwe hatua za kinidhamu maana wamevunja sheria. Kitendo hicho kimewarudisha nyuma na kuwakatisha tamaa watu wengi wanaojishughulisha na sekta ya ajira binafsi. 

Alphonce Madeni,
Mtanda, Lindi.


Barua ya wazi kwa Rais: Askari Magereza tunanyanyaswa 

MHESHIMIWA Rais tunadhulumiwa pesa zetu eti kwa kisingizio cha kuchangia timu ya mpira (Prisons Mbeya). Kuanzia cheo cha Wader (PC) hadi Sergenti tunalipa T.Sh.5,000, Staff Surgent T.Sh.10,000, AssistantInspector T.Sh.20,000, na kuendelea kulingana na cheo. 

Isitoshe tunatengenezewa makosa ambayo adhabu yake ni kukatwa robo ya mishahara; ikizingatiwa kuwa mishahara yetu haikidhi mahitaji. Je mheshimiwa Rais haya unayafahamu? Je vyanzo vya kupatia fedha ni mishahara ya askari? Je adhabu ya askari ni kukatwa robo ya mshahara wake? Je hizi pesa zinapelekwa wapi? 

Kamishna Mkuu baada ya kusikia malalamiko ya askari kwenye vyombo vya habari, ametoa waraka kwa watendaji wake wakuu (RPO's) akielekeza kuwa kutoa mchango wa mpira siyo lazima na asiyetaka asibughudhiwe; lakini la ajabu ni kwamba mwishoni mwa waraka huo anasema, "Hao wasiotaka kutoa ni wakorofi wachache na hivyo ikionekana wengine wanashawishika wachukuliwe hatua." 

Je kauli hii ina maanagani? Je kwani yupo yeyote anayependa kutoa mchango usio na manufaa kwake au familia yake? Je ni mchango gani wa hiyari unapangiwa viwango? 

Mheshimiwa Rais tunaomba kupitia vyombo vyako husika katika dola kulitolea tamko rasmi la kufuta mchango huu, na pia kudhulumu pesa za askari kwa visingizio tofauti. 

Mheshimiwa Rais endapo tutapuuzwa tunaahidi kutoa munkari yetu kwa kutumia silaha tunazopewa kwa ulinzi wa sehemu mbalimbali, kukomesha ukatili na dhulma za hawa viongozi. Tulipofikishwa panatosha, na hatuoni tatizo kutoa roho zao na zetu. 

(Jina limehifadhiwa),
S.L.P. 3042,
Moshi.


Kupotoshwa kwa hijabu nani alaumiwe?
 

Ndugu Mhariri,

Baada ya "mshikemshike" ya aina yake iliyoanza kubeba sura ya aina yake kule bungeni pale baadhi ya wabunge walipoonesha uzalendo wao juu ya dini zao na baadaye kupelekea, Waislamu kupanga maandamano kupinga udini waliouonesha wabunge hao, Rais kwa mdomo wake alikumbusha uhuru walionao Waislamu juu ya vazi la hijabu.

Pamoja na Raiskukumbusha uhuruhuo, badokatika watendaji wa serikali wapo wenye chukibinafsi za kidini. 

Hawakuwa tayari kulitangaza hili bayana na kuliweka katikabaruaza kuwaalika wanafunzi wapya wa Kidatu cha Kwanza na Kidatocha Tano (join instruction) na kuambatanisha taarifa hizo katikaripoti za maendeleo ya mwanafunzi zitolewazokila muhula/mwake. 

Kibaya zaidi walijitokeza watendajiwalioamua kwa makusudi kulipotosha vazila hijabu hususan shule za msingi. Wakawatakawasichana Waislamu wavae skafu (kitambaa cha kichwani) tunasio hijabu kamili. Shati mikonomifupi nasketi ivuke magati kidogo. 

Ndio kusema watendaji hawa walikusudia ninikwa kufanya hivyo? Au walikuwa hawajui hijabu ni nini? Na kama walikuwa hawajui kwanini wasiulize? 

Upande wa pili wazazi, waleziMasheikh na Waislam kwa ujumla tukabweteka kwa kauliya Rias. Hatukufuatiliakuona agizo hilo linatekelezwa vipi. Na pale tulipogundua kasorohatukufuatilia. 

Umefika wakati wa kulifuatilia suala la hijabu upya. Masheikh, maimam, walezi na Waislam wote shimealaykum. 

Abu Firdaus,
S.L.P. 31999,
Dar es Salaam.
 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri:
Serikali itoe hatma ya mauaji ya Mwembechai 

Wanafunzi wa Kiislamu shule za sekondari za serikali Dar wanyanyaswa 

Kanisa liliishinikiza serikali-Waislamu

Sakata ya mabadiliko ya Katiba Zanzibar 

Kukiri kosa na kuomba radhi ndio kipimo cha utu 

HABARI ZA KIMATAIFA 

Ushauri Nasaha  
Kuongoza tabia za watoto 

MAKALA 
Uhuru wa pili na ukombozi wa mwananchi 

MAKALA 
Umuhimu wa uchumi katika Uislam 

Kalamu ya Mwandishi 
Kwa nini kadhia ya Mwembe Chai isifanyiwe uchunguzi? 

Makala 
UPINZANI  OCTOBA 2000 - 3 

MAKALA
MAREKEBISHO YA 13 YA KATIBA YA  JAMHURI YA MUUNGANO: Wananchi Tanzania amkeni 

Riwaya 
Ndoto ya mafanikio 

LISHE 
Vyakula vitupatiavyo mafuta 

Barua/Maoni

MASHAIRI

MICHEZO

  • Tauzany afurahia ligi ya makundi 
  • Kibadeni hakutokomea na fedha za usajili- Milambo 
  • FAT yamuangukia Gama

  •  

     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com


    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita