AN-NUUR 
Na.170 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 9 - 15, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
LISHE
Vitu vinavyoweza 
kuwemo katika vyakula

Na Mujahiid Mwinyimvua 

CHAKULA huwa na sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ni ile inayoliwa na sehemu ya pili ni ile isiyoliwa kamam vile mifupa, ngozi, maganda n.k. 

Sehemu inayoliwa inavirutubisho (viinilishe) ambavyo huuwezesha mwili kukua na kunawili. Virutubisho hivyo kama tulivyowahi kueleza katika makala zilizopita, vinagawanywa katika makundi makubwa sita, makundi hayo ni Kabohaidreti, protini (utomwili), mafuta, vitamini, maji na madini. Kwa vile makundi hayo tulishayaelezea vya kutosha katika makala zilizopita, hapa hatutarudia maelezo hayo. 

Vyakula mbalimbali vina aina tofauti ya virutubisho. Kwa mfano, unga wa mahindi una virutubisho vikuu vya wanga, nyuzi nyuzi (dietary fibres), Protini, madini na vitamini. Nyama inavirutubisho vikuu vya maji, protini, mafuta, madini na vitamini. Nyanya inavirutubisho vikuu vya maji, sukari, na vitamini. Kwa kuzingatia maumbile hayo, wataalamu wa lishe huwashauri wananchi kula aina mbalimbali ya vyakula ili mwili uweze kuvipata virutubisho vyote sita. 

Mbali ya virutubisho, sehemu inayoliwa ya chakula inaweza kuwa na aina nyingine ya vitu ambavyo vinaweza kuboresha au kuathiri afya ya mlaji. Aina moja ya vitu hivyo ni ile inayoitwa "Anti-Nutrients" yaani wapinzani wa virutubisho. 

Mfano wa wapinzani hao ni sumu inayoitwa "Cyanide" ambayo hupatikana katika vyakula kama vile mihogo iliyomichungu. "Cyanide" ni sumu ya hatari kwa sababu inaweza kusababisha kifo kwa muda mfupi. 

Baadhi ya watu wa mkoa Kilimanjaro wanaelewa vizuri zaidi hatari ya mihogo michungu. 

Sumu ya "Cyanide" (uchungu) inaweza kupungua au kuondoka kabisa kama mihogo itatengenezwa kwa njia mbali mbali hasa katika viwanda. Hata hivyo, njia za kienyeji kama vile kutengeneza makopa zinaweza kupunguza kiasi kikubwa cha sumu hiyo katika mihogo. 

Aina ya vitu vingine vinavyopatikana katika vyakula ni ile inayojulikana kama "Anti-Digestive factors" yaani vitu vinavyozorotesha usagaji au unyonyaji wa vyakula tumboni. Kwa mfano, "Phytate" iliyomo katika vyakula vya nafaka inauzuia mwili kunyonya madini ya chuma. Vitu hivyo navyo huondolewa kwa njia mbalimbali hasa katika viwanda vya kusindika/kutengeneza vyakula. Kwa kiwango cha nyumbani, vyakula kama soya na nafaka vilowekwe na viachwe viote kidogo (kama kimea kinavyotengenezwa) na baadaye vikaushwe na kusagwa. 

Vitu vingine ambavyo vinaweza kuwemo ndani ya vyakula tunavyokula ni Pombe (Alcohol) na tindikali (Acids). Vitu hivyo huzalishwa na vijidudu (Yeasts au Bacteria) ambavyo huwemo (kwa njia ya asili) katika vyakula au huingia katika vyakula wakati wa utengenezaji wa vyakula hivyo kiwandani au nyumbani. 

Sambamba na vitu hivyo, vyakula tunavyokula pia vinaweza kuwa navitu vinavyoitwa "Adelitives". Hivi ni vitu vianvyowekwa katika vyakula kwa makusudio maalum kamavile kukiwezesha kukaa kwa siku kadhaa bila kuharibika, kuongeza radha au rangi ya chakula, kuongeza ubora wa chakula (mfano madini joto yanavyowekwa katika chumvi au vitamini C inayowekwa katika juisi au mikate) au kusaidia chakula kutengenezwa kwa urahisi. 

Baadhi ya Adelitives huwa na madhara kiafya kama vile kusababisha kansa. Kwa kuzingatia ukweli huu baadhi ya watu hupendelea vyakula vya asili (si vya kiwandani). Kwa wenye viwanda wazingatie aina na kiwango cha Additives wanachoweka katika vyakula, vingevyo wataathiri afya za wateja wao. 

Pia serikali kwa upande wake iimarishe shirika lake la viwango (TBS) ili kuthibitisha ubora wa vyakula (na bidhaa nyingine). 

Kundi lingine la vitu vinavyoweza kuwemo katika vyakula tunavyokula ni lile lijulikanalo kama Contaminants, yaani vitu vilivyoingia katika vyakula bila kukusudiwa wakati vyakula hivyo vimehifadhiwa au vinatengenezwa au kuandaliwa, kiwandani au nyumbani. 

Kwa mfano karanga ikihifadhiwa mahali kwenye unyenyevu , vijidudu vinaweza kuingia katika karanga na kutengeneza sumu inayoitwa "Aflatoxin" ambayo inadhuru afya. 

Jambo la kufanya ili kukabiliana na "contaminants" ni kuzidisha usafi wa mwandaaji chakula, chombo cha kuhifadhi chakula na mahali ambapo chakula kinahifadhiwa au kinatengenezwa. Vile vile vyakula kama karanga ni vema kuvipika au kuvikaanga. 

 
Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

TAHARIRI 
Tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini ? 

Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri Mkuu ni ya Waislamu 
Na Mwandishi Wetu 

Kuchomwa nyumba za wananchi 
Na Mwandishi wetu 

Maoni Yetu: 
Maisha ya Mtanzania yanapokosa thamani 

Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume 
Na Kassim Juma 

Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu Marekani 
Na Mwandishi Wetu 

Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie mauaji ya Mwembechai 
Na Mwandishi Wetu 

‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’ 
Na Kassim Msuya 

Makala ya Kimataifa 
Nani gaidi: Slobodan Milosovic au Usama bin Laden 
Na Mwandishi Wetu 

Afghanistan washindi dhidi ya uvamizi karne zote 
Na Faiza bint Abubaka 

MAKALA: 
Demokrasia ya rushwa ! 
Na Mwapwani Mohamed 

Tujikwamue na janga la utwaghuti 
Na I. Kikong’ona 

MAONI: 
Nini Jihad na nani Mujahidina ? 

MAKALA: 
Marekani ni magaidi wa haki za binadamu 
Na MUSSA ALLY 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno -2 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

Tusihalalishe mauaji ya raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’ 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya sayansi na tiba 
Na Dk. Amur A.A. 

Msiwageuze watoto ombaomba 
Na H.E. Omar 

MAKALA YA JAMII: 
Profesa Malise Kaisi acha uzushi dhidi ya Mtume Muhammad 

Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana na serikali 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 

Mwembechai wageuka Hame, Bado walindwa na polisi 
Na Badru Kimwaga 

Waislamu Moro waendelea kusaidia wagonjwa 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Mjadala wa Katiba ya Shirikisho kuzinduliwa Dar Jumapili 
Na Mohamed Othman 

Walimu wa dini Tanga wapokea Baiskeli 
Na Abu Said 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya  264 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Vitu vinavyoweza kuwemo katika vyakula 

  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita