AN-NUUR 
Na.170 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 9 - 15, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Waislamu wasisitiza:
Nyumba ya Waziri Mkuu ni ya Waislamu
 
  • Wasema ilitaifishwa kimakosa
  • Wadai serikali iirejeshe na kulipa malimbikizo ya kodi ya nyumba
Na Mwandishi Wetu 

WAISLAMU wamesisitiza kwamba nyumba iliyochukuliwa na Waziri Mkuu ni ya Waislamu na inapaswa kurejeshwa kwa wenyewe. 

Pamoja na kuirejesha, Waislamu wamedai kwamba ni lazima serikali ilipe malimbikizo ya kodi toka ilipoipora nyumba hiyo mwaka 1971. 

Waislamu mbalimbali walioongea na mwandishi wa habari hizi wamesema kwamba zipo nyumba zipatazo 11 za Waislamu katika maeneo ya Upanga n Oysterbay ambazo zimechukuliwa na serikali kinyume cha sheria. 

Moja ya nyumba hizo ni ile iliyopo Oysterbay Plot No. 11 barabara ya Tumbawe ambayo imechukuliwa na Waziri Mkuu. 

Awali, nyumba hiyo ilikuwa mali ya Ali Dewji Gangji wa Singida na baadaye kukabidhiwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ambapo EAMWS ilipovunjwa Kabidhi Wasia Mkuu alikabidhi hati ya nyumba hiyo kwa Bakwata. 

Hata hivyo, imeelezwa kwamba nyumba hiyo pamoja na nyingine zilitaifishwa na serikali mwaka 1971 kinyume cha sheria. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Nyumba za Bakwata Sheikh Yahya Hussein amesema kwamba katika nyumba 11 za Waislamu zilizopo eneo la Upanga ambazo zimeporwa na serikali ni nyumba mbili tu ambazo Bakwata imefanikiwa kuzipata kupitia msaada wa Mh. Mzee Rashid Kawawa. 

Sheikh Yahya Hussein amesema kwamba zaidi ya nyumba hizo 9, kipo kiwanja cha Waislamu kilichopo kona ya Mitaa ya Mkunguni Bibi Titi na Morogoro Road ambacho kimeporwa na kupewa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC). 

Amesema kazi kubwa ya Kamati yake hivi sasa ni kuhakikisha kwamba serikali inazirejesha mali za Waislamu ili mali hizo ziweze kutumiwa katika namna ile ile iliyokusudiwa na wale waliotoa Waqf. 

Zipo taarifa kutoka Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba kwamba serikali inataka kuilipa Bakwata fidia ili ichukue nyumba hiyo iwe ya Waziri Mkuu. 

Hata hivyo, Waislamu hadhaa waliobahatika kuongea na mwandishi wa habari hizi, wamesisitiza kwamba jambo hilo haliwezi kukubalika. 

Kiongozi mmoja ndani ya Bakwata ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini amesema kwamba nyumba hiyo haiwezi kuuzwa. Bali serikali kwanza ilipe malimbikizo ya kodi na kama Waziri Mkuu anaiependa basi aingie mkataba na Bakwata apangishwe. 
 

 
Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

TAHARIRI 
Tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini ? 

Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri Mkuu ni ya Waislamu 
Na Mwandishi Wetu 

Kuchomwa nyumba za wananchi 
Na Mwandishi wetu 

Maoni Yetu: 
Maisha ya Mtanzania yanapokosa thamani 

Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume 
Na Kassim Juma 

Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu Marekani 
Na Mwandishi Wetu 

Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie mauaji ya Mwembechai 
Na Mwandishi Wetu 

‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’ 
Na Kassim Msuya 

Makala ya Kimataifa 
Nani gaidi: Slobodan Milosovic au Usama bin Laden 
Na Mwandishi Wetu 

Afghanistan washindi dhidi ya uvamizi karne zote 
Na Faiza bint Abubaka 

MAKALA: 
Demokrasia ya rushwa ! 
Na Mwapwani Mohamed 

Tujikwamue na janga la utwaghuti 
Na I. Kikong’ona 

MAONI: 
Nini Jihad na nani Mujahidina ? 

MAKALA: 
Marekani ni magaidi wa haki za binadamu 
Na MUSSA ALLY 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno -2 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

Tusihalalishe mauaji ya raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’ 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya sayansi na tiba 
Na Dk. Amur A.A. 

Msiwageuze watoto ombaomba 
Na H.E. Omar 

MAKALA YA JAMII: 
Profesa Malise Kaisi acha uzushi dhidi ya Mtume Muhammad 

Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana na serikali 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 

Mwembechai wageuka Hame, Bado walindwa na polisi 
Na Badru Kimwaga 

Waislamu Moro waendelea kusaidia wagonjwa 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Mjadala wa Katiba ya Shirikisho kuzinduliwa Dar Jumapili 
Na Mohamed Othman 

Walimu wa dini Tanga wapokea Baiskeli 
Na Abu Said 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya  264 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Vitu vinavyoweza kuwemo katika vyakula 

  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita