AN-NUUR
Na.168 Jamadul Akhir 1419, Septembe 24 - Oktoba 1, 1998

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita

 

Mauaji,udhalilishaji Mwembechai:
  • Wanawake Waislamu waandamana Tabora
  • Wamlilia Allah mbele ya Kanisa
  • Wasema ndipo ilikoanzia kadhia ya kuteswa kwao

Na Mwandishi Wetu

MAMIA ya wanawake Waislamu waliokuwa wakiandamana mjini Tabora walisimama kwa muda mbele ya Kanisa la Moravian na kutoa kilio chao kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya wale walioshiriki kuwaua Waislamu Mwembechai na kuwadhalilisha wanawake Waislamu.

Mbele kidogo ya Kanisa hilo kuna Msikiti, Masjid Aziz ambapo pia walisimama na kuwaombea dua mashahidi wa Mwembechai.

Wamesema kwamba katika Kanisa la Moravian ndipo zilipotolewa kauli za kukomesha mihadhara Januari 3 mwaka huu, kauli ambazo zilikuja kuzaa kadhia ya Mwembechai kwa hiyo ni mahali munasibu kutolea kilio chao.

Maandamano ya akina mama hao yalianzia katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mtaa wa Gongoni saa 2:30 asubuhi, kupitia barabara ya Kazima kisha barabara ya Mwanza.

Baada ya kuomba dua mbele ya Kanisa la Moravian, waliendelea kupitia mtaa wa Rufita na kuvuka tena barabara ya Kazima na kuelekea eneo la Ng'ambo ambapo walipita mitaa ya Kitete, Kitunda, Itetemya na kupitia Kituo Kikuu cha Polisi Tabora mpaka Msikiti wa Shirika la Reli.

Kutoka hapo waliingia tena barabara ya Kazima. Wanawake hao waliobeba mabango yaliyokuwa na ujumbe maalum kwa wahusika, walimalizia maandamano yao katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa saa 5:30 asubuhi ambapo lilifanyika kongamano.

Mwisho wa kongamano hilo wito ulitolewa kwa Waislamu kote nchini kuutumia vizuri uhuru wao wa kupiga kura vinginevyo watakuwa wanajidhuru wenyewe kama mshumaa. Mshumaa unaowaangazia wengine huku wenyewe ukijiunguza na kujimaliza.

Hayo yamesemwa na Sheikh maarufu mjini Tabora Sheikh Ali Salala wakati akifunga kongamano hilo Septemba 20, mwaka huu.

Wito huo wa Sheikh Salala umekuja kufuatia mada mbalimbali na mjadala katika kongamano zilizoonyesha kwamba ipo dhulma inayofanywa dhidi ya Waislamu na viongozi wa kisiasa ambao wamepata madaraka kupitia kura za wananchi.

Pamoja na wito huo, wanawake Waislamu waliokutana katika kongamano hili walikariri kilio cha Waislamu kwamba waliowaua Waislamu pale Mwembechai wafikishwe mahakamani.

Aidha, waliazimia kuimarisha elimu kwao na watoto wao ikiwa ni pamoja na kudumisha maadili ya Uislamu.

Walimtaka kila mwanamke Muislamu atambuliwe kwa kitambulisho chake cha Hijab na kuwalaani wale wote wanaokiuka maadili kwa kujichubua nyuso zao na kubadili nywele.

Waliwaomba Masheikh wawe imara katika kusimamia maadili ya Kiislamu na kuwataka wasishiriki kufungisha ndoa zenye ngoma na mambo mengine yaliyo kinyume na Uislamu.

Juu 
 

YALIYOMO  
 
TAHARIRI 
Iran ina agenda gani?

Mauaji,udhalilishaji Mwembechai: Wanawake Waislamu waandamana Tabora Na Mwandishi Wetu

BUCHA YA NYAMA YA NGURUWE KATIKATI YA WAISLAMU
Na Mwandishi Wetu

'Serikali ieleze hatua iliyochukua kuhusu mauaji Mwembechai'
Na Kassim Juma

Vijana wa Kiislamu wajiimarisha Bukoba
Na Nooh Mustafa, Bukoba

Sheikh Mzonge awataka Waislamu Moshi wasimamishe swala
Na Ashraf Yussuf, Moshi

TAMKO LA PAMOJA LA MISIKITI SABA YA MWANZA-KUPINGA OMBI LA BAKWATA KWA SERIKALI LA KUIFUTIA USAJILI WAKE

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 7

MAKALA: Baadhi ya Watanzania wangali wanaishi ‘Tanganyika’
Na Mwandishi Wetu

HOJA BINAFSI: Maendeleo ya Tanzania ni ndoto
Na Fatma Mussa

‘Musiwasingizie wake zenu maovu’
Na Habiba Swedi, Arusha

Wanafunzi Waislamu Songea wapata viongozi
Na Mwandishi Wetu, Songea

Kikundi cha wanawake wa Kiislamu Bi. Khadija – Dodoma
Na Abu Zuberi, Dodoma

Waahidi kutekeleza majukumu kwa jina la Allah
Na Habiba Swedi, Arusha

Arumeru wahitaji Da’awa
Na habiba Swedi, Arusha

Wanawake wa Kiislamu wazungumzia maendeleo yao

Kauli ya wanawake wa Kiislamu Iringa kuhusu kadhia ya Mwembechai

Uislamu ulivyoingia Zanzibar

Wanawake Singida walaani mauaji Mwembechai Wamchangia Mama Chuki 17,000/-
Na Mwandishi Wetu

Sekondari ya Kiislamu kujengwa Maere Tanga
Na Abu Abdullah, Tanga

Sheikh ahimiza Waislamu Lindi wafuate mafunzo ya Uislamu
Na Mohamed Mussa, Lindi

Sheikh Zuberi awataka Waislamu Dodoma kuimarisha Misikiti
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mafundisho ya Quran 
Dhikiri maana yake nini? - 2

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Matatizo ya tumbo yanayosababishwa na utumiaji wa maziwa

Matangazo 

 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org  

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita