Na.175 Rajab 1419, Novemba 13 - 19, 1998 |
WAZO mpachiko ni wazo linalopachikwa katika akili ya mtu hadi linakuwa ni sehemu ya dhana au imani ya mtu huyo. Mara nyingi wanaopachika watu mawazo huwapachika wakiwa wadogo, na kuhakikisha kuwa wanaopachikwa wanakuwa (kiumri) na wazo hilo. Inawezekana pia kwa mtu mzima kupachikwa wazo. Mfano mzuri wa wazo mpachiko ni lile wazo waliopachikwa watu wakawa na dhana ya kumuona tajiri kama mtu mbaya, na kumwita bepari, mlanguzi, kupe, bwanyenye na kadhalika, hadi watu wakaogopa kuwa matajiri. Kwa jinsi utajiri ulivyochukuliwa kama ni dhambi, baadhi ya "watuhumiwa" walidiriki hata kutupa mali zao baharini. Mara nyingine mtu huweza kugundua kirahisi tu kuwa wazo alilonalo ni mpachiko, na huliacha, kama halina mantiki. Kwa mfano, wengi tulipachikwa dhana kuwa ukimuona mama yako ana mtoto mchanga, basi ujue kanunua, labda dukani, sokoni au hospitali, au kamuokota. Baadaye, dhana hii hutoweka na tunatokea kujua watoto wanavyopatikana. Leo ninaleta wazo mpachiko lililowajaa mamilioni ya watu, wengine ni maprofesa wenzangu. Hebu angalia picha iliyopo hapo. Wengi wetu tunamuona mtu aliyelala chali akiwa yuko uchi. Pengine wasomaji wengi watashangaa kwa nini Sa Changwa leo kaweka picha mbaya ya mtu ambaye hajajistiri. Sina ajenda ya siri naomba univumilie kidogo. Angalia nukta zilizowekwa kuizunguka picha hiyo, halafu chukua kalamu uchore mistari kuunganisha nuka moja hadi nyingine kwa mfuatano wa namba, kuanzia moja, mbili, tatu na kuendelea. Hapo utagundua kwamba dhana ya mwendauchi aliyelala chali inaondoka, inakuja dhana ya mtu mtakatifu, ambaye wengi humwita mwokozi. Dhana hii ya pili ikishakuja, kwa wengi ile dhana ya mtu katundikwa kwenye mbao akiwa uchi inaondoka. Kwa wengine, mwendauchi yule hubadilika kuwa mungu wao. Kwa wale wenzangu wanaoamini kuwa kufufuka kupo, tujaribu kupiga picha, huyu jamaa akifufuka, halafu akakuta masanamu na picha zake akiwa katundikwa, yuko uchi, karaliwa shingoni, na anaitwa mungu, hivi atajisikiaje? Ili kutuweka huru na wazo hili mpachiko, Mwenyezi Mungu anatumbia: "Na hawakumuua wala hawakumsulubu..." (Qur. 4:157)
|
YALIYOMO
Maoni Kuvuja kwa mitihani: Tuweni wakweli kwa nchi yetu Katibu
wa Baraza Kuu azikwa Dar
Ubabe
wa madhalimu kuzimwa:
MACHO
YA SHUTUMA
Wazo
mpachiko (Programmed mind)
Ta'azia: Abbas Shaaban Kilima 1938-1998 Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 4
Siri
ya Miujiza
Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo
Ifahamu
Madrasat Ghazal Muslim - Moro
Pamoja
na sala, tusimamishe zakah
Aina
za maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu
Israi
na Miiraji ni miujiza
Pamoja
na ahadi ya Serikali kuzifuta: kesi za mihadhara zaendelea mahakamani
Waislamu Uluguruni Moro wazama kwenye matambiko Imarisheni
miradi ya elimu - Prof. Mikidadi
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (5)
Mafunzo
ya Qur'an
Chakula
na lishe
|