Ramani ya kisiwa cha Pemba

Kuhusu Jumuia

Wasiliana nasi

 

Kwa taarifa au maelezo yoyote kuhsu Jumuia, tuandikie kwa e-mail: tahfidhpemba@gmail.com

Jumuia ya kuhifdhisha Qur’an Pemba ilianzishwa rasmi mwishoni mwa mwaka wa 2006.

 

Kuanzishwa kwa jumuia hii kumetokana na juhudi za watu binfsi za kuhifadhisha Qur’an kwa vijana wa Madrasa zilizoanza tokea mwishoni mwa miaka ya 80. Juhudi hizo zilianza kuzaa matunda mwanzoni mwa miaka ya 90 alipopatikana mwanafunzi wa kwanza aliyehifadhi Qur’an kamili.

 

Kuanzia miaka hiyo ya 80, kazi ya kuhifadhisha Qur’an iliendelea lakini kwa kasi ndogo kutokana na kukosekana kwa uongozi wa kuwahamasisha vijana na pia kuwapa motisha walimu kwa ajili ya kuendeleza kazi hiyo ngumu. Kwa wakati huo zilikuweko jumuia nyingi ndogo ndogo, kama vile jumuia za wilaya na jumuia za vijiji. Kubwa waliloweza kulifanya ni kuratibu mashindano ya vijiji mara moja kwa mwaka baada ya wana kijiji kuchangishana. Hata hivyo, haya yalikuwa yanafanyika katika baadhi ya vijiji na kushindikana katika vijiji vyengine kutokana na hali ngumu za kimaisha.

 

Kutokana na hali hii, vijana walikosa motisha wa kuindelea kuhifadhi. Na wengi wa vijana hawa walikatisha mazoezi ya kuhifadhi pamoja na kuwa baadhi yao walikuwa wamehifadhi zaidi ya juzuu kumi.

 

Harakati za kuhifadhi Qur’an zilipata msukumo pya mnamo mwaka wa 1996 wakati Sheikh Suleiman Ally Yussuf aloporudi kutoka masomoni chuo  kikuu cha Madina. Sheikh Sukleiman alifanya juhudi ya kutembelea baadhi ya vyuo vinavyohifadhisha Qur’an ili kujua kazi inaendelea vipi, na ni matatizo gani yanayowakabil wanafunzi na walimu. Aliweza kubaini kuwa tatizo kubwa lilikuwa ni kukosekana kwa motisha; mbali na kuwepo matatizo mengine mengi yaliyowakabili walimu pamoja na wanafunzi wao, ambayo yanaeleweka na watu wengi. Haya ni pamoja na ukosefu wa mwahala muzuri mwa kufanyia kazi na vifaa vya kaze wenyewe, ikiwemo misahafu.

 

Baada ya tathmini hiyo, ndipo alipoanza juhudi mbali mbali za kuwahamasisha walimu na wanafuzi. Mafanikio yalianza kupatikana na kupelekea kuandaliwa mashindano ya Qur’an kwa vijana ya Pemba nzima. Mashindano yalianza katika mwaka wa 2002 bila ya kuwa chini ya mwevuli wa jumuia yoyote. Ilipofika mwaka wa 2006 ndipo ilipokuja fikra ya kuanzisha chombo maalum kitakachounganisha juhudi zote za fani ya kuhifadhi Qur’an. Ndipo Jumuia ya kuhifadhisha Quran Pemba ikaundwa ikiwa chini ya ulezi wa Sheikh Suleiman. Na kwa uwezo wa Allah Jumuia ikafaniliwa kusajiliwa mwaka uliofuata wa 2007.

 

Jumuia imesajiliwa kwa jina la TAHFIDH-LQUR’AN PEMBA. Namba zake za usajili ni 0141212000232.

 

JUMUIA YA KUHIFADHISHA QUR’AN PEMBA

æóáóÞóÏú íóÓøóÑúäóÇ ÇáúÞõÑúÂäó áöáÐøößúÑö Ýóåóáú ãöä ãøõÏøóßöÑò