Mbunge wa Kibaha Dk. Ibrahimu Msabaha amelaani mauaji yaliyofanywa na
Polisi dhidi ya Waislamu na
kusema kwamba kama Mbunge hawezi kukaa kimya wakati watu wanauliwa.
Akizungumza jimboni kwake hivi karibuni Dk. Msabaha ameeleza kwamba
Polisi haruhusiwi kuua. Bali
inatakiwa kumkamata muhalifu na kumfikisha katika vyombo vya sheria.
Maelezo haya ya Dk. Ibrahim Msabaha yamekuja baada ya kutakiwa na mwananchi
mmoja katika jimbo lake
aeleze ni kwanini anazungumzia mambo ya Mwembechai wakati si jimbo
lake.