Kampeni za kueneza kondom

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imetakiwa isishiriki kufanya biashara na roho za watu kwa hatua yake ya kuendeleza kampeni ya matumizi ya kondom kama kinga ya ukimwi.
 
Hayo yamesemwa na watalaamu mbalimbali kufuatia uzinduzi wa kampeni ya kudhibiti ukimwi ambayo itadumu hadi Desemba.

Wakiongea na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Morogoro na Dar es Salaam, watalaamu na washauri juu ya magonjwa ya kuambukiza wamekiri kwamba katu kondom si kinga ya ukimwi na kuongeza kwamba hali hivi sasa ni mbaya sana na watu watazidi kupukutika kama wataendelea kupumbazwa kwamba kondom ni kinga ya ukimwi.

Washauri hao wamesema kwamba kondom zimo nchini kwa muda mrefu sana na kwamba utafiti umeonyesha kwamba zoezi la kuwahamasisha watu watumie kondom limefanikiwa sana kwani matumizi ni makubwa Inaendelea Uk. 3Inaendelea Uk. 3SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Sheikh Omar Mohammed Bafadhil akihutubia waumini katika moja ya Misikiti ya Jijini.sana.

Wanasema kwamba ripoti kutoka maduka ya madawa, nyumba za wageni (guest houses), mabaa n.k. zimeonyesha kiwango kikubwa cha ununuzi na matumizi ya mipira hiyo.

Hata hivyo, wamesema matumizi hayo makubwa ya mipira yamekuwa kana kwamba ni kiongeza kasi cha kuenea kwa virusi vya ukimwi.

Mmoja wa washauri hao akitoa mfano alisema kwamba ni watu wawili tu kati ya kumi wanaokuja kwake kutaka ushauri ambao hujikuta wazima (-ve). Na kwamba kila siku hupokea wagonjwa au watu wenye wasiwasi kwamba wameambukizwa HIV wasiopungua saba (7).

Mtaalamu na Mshauri huyo ambaye kituo chake cha kazi kipo Morogoro Mjini, amesema kwamba tatizo kubwa hivi sasa ni kwamba wakubwa serikalini wameamini kwamba kondom ni kinga ya ukimwi na wanawahamasisha wananchi wawape kondom mpaka watoto wao.

Kwa hali hiyo, amesemawatu wa chini hawawezi kutamka hadharani kauli iliyo kinyume na sera na msimamo wa serikali.

Na kuongeza kwamba suala hili limeingiliana na maslahi ya kibiashara. Aidha, ni kwa kuzingatia msimamo na imani hiyo ya serikali, watoa ushauri nasaha wote walioongea na mwandishi wa habari hizi walikataa kutajwa majina yao gazetini.

Hata hivyo, walisisitiza kwamba ufumbuzi wa hali hii ni wananchi wenyewe kuja juu na kuitaka serikali iache kuwadanganya juu ya matumizi ya kondom kama kinga ya ukimwi.

Mama mmoja ambaye ni mmoja wa washauri alisema kwa masikitiko kwamba anaona huzuni na uchungu kuona jinsi wananchi wanavyoswagwa na kuuvamia ukimwi kwa kufuata imani potofu za "uzinzi salama". Mama huyo ambaye aliyasema haya alipoongea na mwandishi wa habari hizi mjini Morogoro Juni 3, alisema kwamba maadhali watu wanaendela kukiuka amri ya Mungu juu ya uzinzi si kondom wala chochote kitakachosaidia kutosambaa kwa ukimwi.

Aidha, alilaani tabia ya watu kuvaa dini na kumjua Mungu wanapokwenda Makanisani na Misikitini, lakini wakitoka hapo hubuni njia zao za kijahili kushindana na Mungu.

Utafiti wa gazeti hili umegundua kamba watu wengi wanaokwenda kupata ushauri na kupimwa HIV ni wale ambao ama wamefiwa na wapenzi wao wenye dalili za ukimwi, wanawake wanaotaka kushika mimba, ambao mimba zao hutoka (abortion) au wanawake wanaofiwa na watoto wao wadogo wanaoonyesha dalili za ukimwi.

Ni katika kundi la watu hao ambalo mtaalamu mmoja mjini Morogoro amesema kwamba ni watu wawili tu kati yao hukutwa wamesalimika.

Na kwamba kasi ya watu wanaokwenda kwenye vituo vya ushauri wenye matatizo ama ya kufiwa na wapenzi wao au wanawake kufiwa na watoto wachanga wenye dalili za ukimwi ni ya kutisha.

Amesema imefika wakati wananchi wenyewe wajinusuru kwa kuacha kusikiliza propaganda za "uzinzi salama" na kuitaka serikali iache kutumia vyombo vya habari vya umma (RTD) kuwaangamiza wananchi kwa kutangaza biashara ya "Salama"

"Salama ya wananchi ipo kwenye maadili na wala sio kwenye "Salama Kondom" kama wananchi wanavyohadaiwa", alisema.

Akimalizia imaoni yake alisema tatizo kubwa ni ujinga na kisomo kidogo. "Lau wananchi walio wengi wangejua "vijitundu" katika kondom